Social:

RSS:

Vatican Radio

The voice of the Pope and the Church in dialogue with the World

language:
Vatican Radio

Home / Church

Msalaba ni kielelezo cha ushujaa wa Yesu na mashahidi wa imani


Fumbo la Msalaba linayagusa maisha ya mwamini kwa namna ya pekee. Msalaba katika mapokeo ya kale, ilikuwa ni alama ya uovu wa kutisha na hali ya kukatisha tamaa, lakini, kwa njia ya Yesu Kristo Mkombozi wa dunia, Msalaba umepata maana mpya katika maisha ya mwanadamu; sasa ni kielelezo cha ushujaa wa Yesu na mashahidi wa imani wanaoendelea kuyamimina maisha yao kwa ajili ya imani yao kwa Kristo sehemu mbali mbali za dunia.

Ni ishara ya mapendo, neema, sala, msamaha na matumaini. Ni kutokana na maana hii mpya Mama Kanisa anaona fahari kuu kuutangaza utukufu na kuimba sifa kuu za Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Msalaba unaendelea kumfunza mwamini kwamba, hakuna mapendo kamili yasiyokuwa na mateso na matumaini ya uzima wa milele.

Changamoto kwa waamini katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo ni kuuangalia, kuutafakari, kuushangaaa, kuusikiliza, kuheshimu, kuutukuza na kuuabudu kwa imani, matumaini na mapendo, kwani ni kielelezo cha wokovu wa dunia.

Kimsingi, Mama Kanisa ataadhimisha Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba hapo tarehe 14 Septemba, 2009, baadhi ya Mabaraza ya Maaskofu Mahalia wanapenda kuiadhimisha Siku kuu hii jumapili ijayo, ili kutoa fursa kwa waamini kuweza kushiriki vyema. Ndani ya nyumba, tunaye Mheshimiwa Padre Gosbert Byamungu, kutoka Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo, akitumegea cheche za Neno la Mungu katika adhimisho la kutukuka kwa Fumbo la Msalaba. RealAudioMP3