Social:

RSS:

Vatican Radio

The voice of the Pope and the Church in dialogue with the World

language:
Vatican Radio

Home / Church

Mons. Mupenda watu Katibu Mpya wa Baraza la Kipapa kwa Wahudumu wa Afya.


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, amemteua Mons. Jean Marie Musivi Mupendawatu, kuwa Katibu wa Baraza la Kipapa, kwa ajili ya wahudumu wa Afya. Hadi uteuzi huu, alikuwa ni Katibu msaidizi katika Baraza hilo.

Wakati huohuo Papa akamteua Padre Augusto Chendi , kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mons Mupendawatu. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Afisa katika Ofisi za Shirika kwa ajili ya mafundisho ya imani sadikifu.

Mons. Jean-Marie Mate Musivi Mupendawatu , alizaliwa Lubero, Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo , hapo 18 Julai 1955.
-Alipata masomo yake kwanza katika seminari ndogo ya jimbo la Musienene, na masomo ya filosofia e teologia katika Seminary kuu ya "Pio X" ya Bukavu na baadaye katika Chuo Kikuu cha "Yohane Paulo Paolo II" cha Kinshasa.
-
Alipadrishwa 26 agosto 1982 katika jimbo la Butembo-Beni (Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo). Baada ya hapo akawa Mwalimu katika seminari ndogo ya Musienene na Mkuu wa seminari hiyo (1982-1985); Pia aliwahi kuwa Kasisi katika Kituo cha Afya huko Canada , "Centre Hospitalier de Verdun" na kituo kwa ajili ya matunzo ya Wazee, "Hôtel-Dieu de Montréal".
Tangu 1985 hadi1989 akawa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Urbaniana, ambako alijipatia shahada ya udaktari katika sheria za Kanisa.

    1° aprile 1991, alianza utume wake katika huduma za Jimbo Takatifu kama afisa katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wahudumu wa Afya, na hapo 31 Julai 2009 aliteuliwa na Papa kuwa Katibu Msaidizi katika baraza hilo
  • Na pia alikuwa ni mjumbe katika Bodi ya Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Elimu ya Maisha. Na ni mwandishi wa mada mbalimbali zinazohusiana na mada za “bioethics”

  • -Anazungumza: Kifaransa, Kiitaliano, Kiingereza na Kiswahili.